Msanii wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz na Nandy leo, April 19, 2018 wamefika katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA), kujuzwa mambo kadhaa kuhusu sheria za mitandao.
Diamond amefika TCRA mara baada ya kuweka video zisizo za maadili mtandaoni ambapo ameomba radhi kutokana na kitendo hicho.
Diamond amefika TCRA mara baada ya kuweka video zisizo za maadili mtandaoni ambapo ameomba radhi kutokana na kitendo hicho.
“Na mimi ni miongoni mwa mabingwa wa kiki, najikubali, najua kabisa drama ninazo kila siku lakini tunaziweka vipi zisiende kuwatia dosari viongozi ambao wanapambana kuhakikisha sanaa yetu inafika mbali,” amesema Diamond.
“Kwa sababu ikienda kwa mazingira ambayo yalikuwa yamezoeleka huko nyuma unawavunja moyo viongozi ambao wanapigania sanaa ifike mbali,” amesisitiza.
Hivi karibuni, Waziri wa Habari, Sanaa na Utamaduni, Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza Bungeni aliangiza Diamond na Nandy kuhojiwa kuhusu kusambaa kwa video zao zinazokiuka maadili, wasanii wote walisharipoti katika kituo kikuu cha Polisi Dar es Salaam.
Tiada ulasan:
Catat Ulasan