Mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba imeingia kandarasi ya miaka miwili na aliyekuwa kiungo wa Mtibwa Sugar ya Morogoro, Hassan Dilunga.
Kabla ya kutua kwa mabingwa hao wa msimu wa mwaka 2017/18, Dilunga amehusishwa na kutakiwa na klabu yake ya zamani ya Yanga.
Hata hivyo usajili huo ulikuwa na mvutano wa hapa na pale baina ya Simba dhidi ya Mtibwa juu ya usajili wa Dilunga ambapo waajiri wake hao wa zamani Mtibwa lakini pande hizo mbili zimefikia makubaliano.
Katika kuonyesha inakuwa na uhai wa safu ya kiungo Simba SC mpaka sasa inao wachezaji Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Mzamiru Yassin, Said Ndemla na wengineo.
No comments:
Post a Comment