Miezi ya hivi karibuni kumekuwa na maneno mengi mitandaoni wengi wakilaumu uongozi wa WCB kuwa wanamfanyisha show nyingi Diamond Platnumz kiasi kwamba mwili wake unaporomoka kila siku huku wengine wakienda mbali zaidi kuwa kukonda kwake ni kutokana na kuvurugiga kwa mahusiano yake na mzazi mwenzie Zari.
Sasa Uongozi wake kupitia kwa meneja Babu Tale ameeleza sababu za Diamond kupungua mwili kwa muda mfupi kuwa ni kukosa muda wa kulala kutokana na jukumu zito la ujio wa Wasafi TV.
Babu Tale amesema kuwa Diamond kila siku anapambana kwa ajili ya kukamilisha malengo yake ya baadae ikiwemo kuiimarisha Wasafi TV.
“Kuna baadhi ya watu wanasema msanii wangu anapungua mimi na nenepa navimba, Kama hamjui Media sio kitu kidogo, wakati tunaanza tulijua ni kazi ndogo, kwa miezi sita non stop msanii wangu analala masaa mawili tu, kwa sababu ya kuandaa hiki mnachokiona machoni mwenu.. Wiki mbili za mwanzo tukawa tunakasirika kwa nini anafanya kazi ngumu, ilipofika mwezi tukawa tunaona ana-loose weight (kupungua uzito) na bado kazi zinaendelea tukawa tunashangaa ana nia gani huyu?,“amesema Babu Tale kwenye mkutano wake na Waandishi wa Habari uliofanyika leo Juni 19, 2018 katika ukumbi wa Slipway.
Awali dada wa Diamond Platnumz, Esma alinukuriwa kwenye mitandao ya kijamii akidai kuwa Diamond anapungua kwa stress za kuachana na mzazi mwenzie, Zari.
Diamond Platnumz ambaye ndiye Mkurugenzi wa WASAFI TV leo ameongeza rasmi Channel yake kwenye king’amuzi cha StarTimes.
No comments:
Post a Comment