Wikiendi iliyopita msanii Alikiba alifunga ndoa na mwanamke kutoka nchini Kenya ambapo kati ya wasanii waliomtakia kheri siku ya ndoa yake ni msanii mwenzie Diamond Platnumz ambae watu wengi hawakuamiani kama angeweza kumpa hongera hizo.
Dada wa msanii Diamond anaejulikana kwa jina la Esma Platnumz, alifunguka na kuandika katika ukurasa wake kuwa anamuonea wivu sana dada ayke na Alikiba kwa furaha aliyonayo kuona kaka yake anaoa.
Akiongea tena kwa mara nyingine katika viwanja vya Leaders club , Esma anakiri kuwa ni kweli amekuwa akimuonea wivu kwa sababu hata yeye anatamani sana kaka yake awe na mke mmoja wa halali na siokuchepuka kila siku na pia kaka yake akioa hiyo itawapa wao nguvu kwa sababu wamekuwa wakitukanwa sana na watu kutokana na tabia ya kaka yao kubadilisha wanawake lakini hawana cha kufanya.
"sisi hatuna kosa kwamba ukiletewa mtu ukasema huyu simtaki, inabidi umkubali tu, sasa anapooa unakua u ajua kabisa kuwa huyu ndo wa halali kwaio unakuwa na nguvu ya kusema kwanin upo na huyo wakati huyu yupo.nilijisiakia wivu kwakweli na hata nilivyoandika niliandika huku nikiwa nasisimuka mpka nywele"
No comments:
Post a Comment