Msanii Naseeb Abdul Maarufu kama Diamond Platnumz amefikishwa Polisi jana kuhojiwa kutokana na kusambaza kwa video zake zisizo na maadili katika mitandao ya kijamii
Hayo yamesemwa na Waziri wa Habari, Michezo, Utamaduni na Sanaa Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa Bungeni wakati akijibu swali juu ya kanuni za maudhi ya Mitandaoni alilouliza Mbunge Goodluck Mlinga
Aidha, Waziri Mwakyembe amesema Msanii Faustina Charles(Nandy) naye amefikishwa Polisi kuhojiwa kufuatia video yake ya faragha akiwa na Msanii mwenzake Billnass kusambaa mitandaoni
Waziri Mwakyembe amesema kwa sasa wanaangalia taratibu za kuwafikisha Mahakamani.
No comments:
Post a Comment