HABARI BURUDANI MICHEZO UDAKU AJIRA MUZIKI NA MENGINE MENGI KWENYE UKURASA HUU

  • Breaking News

    Friday, April 20, 2018

    Mrembo Agness Gerald ‘Masogange’ afariki dunia

    Mwanamitindo na video queen marufu bongo Agnes Gerald maarufu kama Masogange, amefariki dunia leo kwa tatizo la nimonia na upungufu wa damu..





    Akithibitisha taarifa ya kifo hicho muigizaji mkongwe Steve Nyerere amesema kwamba  Agnes amefariki muda mfupi huu akiwa hospitali ya mama Ngoma Mwenge, na hivi sasa wanapeleka mwili hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
    Agnes Masogange alikuwa maarufu baada ya kuonekana kwenye video kadhaa za bongo ikiwemo Masogange ya Belle 9


    Taarifa za kifo hicho zimethibitishwa na ndugu wa karibu na marehemu, Dick Sound ambaye amesema mwili wa marehemu unasafirishwa jioni hii kwenda kuhifadhiwa mochwari- Muhimbili.
    Wiki tatu zilizopita marehemu alishindwa kuhudhuria mahakamani kusikiliza kesi iliyokuwa ikimkabili kwa kulazwa hospitalini, hii ni kabla ya kesi hiyo kutolewa hukumu wiki iliyopita.
    Mastaa mbalimbali wa muziki na waigizaji wa filamu wametoa pole kufuatia taarifa hizo za mshtuko za kifo hicho, na habarizero.com inatoa pole kwa familia yake katika kipindi hiki kigumu.
    Taarifa zaidi juu ya msiba huo tutakuletea kaa nasi karibu.

    =========
    UPDATES:
    =========

    Video queen maarufu Bongo Agness Gerald maarufu kama Agness Masogange amefariki Dunia leo katika Hospitali ya Mama Ngoma Mwenge jijini Dar Es Salaam.

    Alikuwa anasumbuliwa na nimonia pamoja na tatizo la kupungukiwa na damu.

    Mungu ailaze roho yake mahala pema peponi.


    No comments:

    Loading...

    AJIRA

    SIMU

    AFYA

    UDAKU