Msanii maarufu wa muziki duniani, Beyonce amenunua jengo la kanisa kongwe mjini New Orleans nchini Marekani.
Kanisa hilo ambalo limejengwa kwa mawe miaka ya 1900’s limemgharimu Beyonce kiasi cha dola $850,000 sawa na tsh bilioni 1.9 .
Kwa mujibu wa taarifa kutoka mitandao mbalimbali ya burudani duniani ikiwemo TMZ na Shaderoom zinaeleza kuwa lengo la kununua kanisa hilo ni kueneza dini yake ya Beyism.
Beyism ni dini ambayo wafuasi wake wanamsujudu Beyonce kama mungu wao na tayari imeshapata maelfu ya wafuasi nchini Marekani.
Mwaka 2014, waumini wa dini ya Beyism walianzisha kanisa la rasmi la Beyonce walilolipa jina la ‘The National Church of Bey’ huko mjini Atlanta nchini Marekani.
Waumini wa Kanisa hilo wanaimba nyimbo za Beyonce na kusoma biblia maalumu zinazoitwa beyble.
Kanisa hilo la Beyonce limepambwa na picha nzuri za Beyonce akiwa amevalia mavazi ya nguo kama za viongozi wengine wa makanisa ya kikristo.
No comments:
Post a Comment