China imetupilia mbali ukosoaji wa Marekani juu ya madai yake kuwa mashirika ya ndege 36 ya kigeni, yakiwemo Makampuni ya Marekani, kuacha kutumia vielelezo vinavyoeleza kuwa Taiwan, Hong Kong na Macau haziko chini ya utawala wa Beijing.
Uongozi wa Usafiri wa Anga wa China umepeleka ujumbe juu ya hilo kwa mashirika hayo ya ndege Aprili 25.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nje (Geng Shuang) amesema Jumapili “mashirika yakigeni yanayoendesha shughuli zake China ni lazima yaheshimu uhuru wa China na maeneo ya nchi yake, wafuate sheria za China na kuheshimu hisia za kitaifa za watu wa China.”
White House Jumamosi imelaani kile ilichokiita ni ‘upuuzi wa Orwellian wa China,’ wakitumia mfano wa mtunzi wa simulizi za kitabu cha Kiingereza na dira yake juu ya mustakbali wa taifa la kidikteta katika kitabu hicho mwaka 1984. White House imesema hatua hiyo ya China “ni sehemu ya muelekeo wa kuhodhi maoni yake ya kisiasa kwa raia wa Marekani na makampuni binafsi,’ na kuitaka iache vitisho vyake na ubabe.
Geoffrey Thomas, mhariri wa tovuti inayofanya tathmini ya mashirika ya ndege yenye makao yake AirlineRatings.com website, ameiambia VOA kuwa huu ni mgogoro wa kisiasa akielezea juu ya hisia kali zilizotolewa na Marekani.
Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani Jumamosi imesema kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo na mjumbe wa Kamati Kuu ya Siasa ya chama tawala cha China Yang Jiechi, katika mazungumzo ya simu, wamekubaliana ‘umuhimu wa kujenga mahusiano yenye tija baina ya mataifa hayo mawili.
No comments:
Post a Comment