Mrembo ajulikanaye kwa jina la Rebecca Barker kutoka nchini Uingereza amejikuta akirejesha furaha katika maisha yake baada ya kuishi maisha ya tabu kwa miaka sita mfululizo, ambapo katika kipindi hicho alikuwa hawazi jambo lingine lolote kichwani mwake zaidi ya kufanya mapenzi au kushiriki tendo la ndoa.
Rebecca (37) mwenye watoto watatu kupitia kipindi cha Victoria Derbyshire kinachorushwa na kituo cha runinga cha BBC amesema kuwa tatizo la kupenda ngono kupita kiasi lilianza kumtokea mwaka 2012 akiwa na miaka 31 muda huo akiwa na mume wake wa kwanza ambaye ndiye baba watoto wake.
Akizungumza kwenye kipindi hicho cha masuala ya mahusiano, Rebecca anasema ilifikia hatua hata kazi alikuwa hapendi na alikuwa akimlazimisha mumewe abaki nyumbani kwa ajili ya shughuli hiyo.
Hata hivyo, Rebecca amesema baada ya kutengana na mumewe kwa miaka miwili alifanikiwa kuishi na wanaume watano lakini wote walimkimbia na kwa sasa amerudiana na mzazi mwenzie baada ya kupata matibabu ya Kisaikolojia.
“Nilitamanani kila wakati kufanya mapenzi kitu ambacho kilikuwa ni kigumu kwa kweli, hata nilipojaribu kujizuia nilishindwa kwani haikupita hata dakika tano nilitamani kushiriki tendo la ndoa. Nadhani ilitokana na shinikizo la mawazo sikuwa nawaza jambo lolote kila nilipoamka kitandani niliwaza ngono tu hata hamu ya kula sikujisikia.“amefunguka Rebecca.
“Sikuridhika kabisa kufanya mapenzi mara tano au sita kwa siku niliona kama nahitaji kufanya mapenzi kwa masaa yote 24 niliumia sana kwani nilijihisi mpweke, sikuwa natoka nyumbani kwa sababu nilikuwa naona aibu, nilikuwa nikifikiria kufanya ngono kila wakati. Hata iwapo hakuna mtu ambaye angeweza kugundua kilichokuwa katika fikra zangu , niliona kama anajua mawazo yangu.“amesema Rebecca.
Bi. Rabecca amesema kabla ya kuchukua maamuzi ya kurudiana na mzazi mwenzake alienda kwanza kwa wazazi wake ndipo alipopata mawazo ya kwenda kwa wataalamu “Nilikuwa chini ya uangalizi wa mtaalamu wa matatizo ya kiakili wakati huo ambaye alikuwa akinimbia kwamba atanibadilisha na kweli mpaka sasa najiona mwenye furaha“.
Akielezea tatizo hilo lilikotokea baada ya kupata maelezo kutoka kwa madaktari hao, Bi. Barker amesema alipatwa na shinikizo la kiakili mwaka 2012 baada ya kujifungua mtoto wake wa tatu na kipindi hicho alikaa mbali na mumewe kwani alienda kuishi Ufaransa kikazi.
Kwa upande mwingine, Bi. Rebecca ameiombaa Mamlaka ya Afya nchini Uingereza (NHS) kushirikiana na Shirika la Afya ulimwenguni (WHO) kuchukulia tatizo la uraibu wa ngono kama uraibu mwingine wa madawa ya kulevya kwani ni tatizo kubwa ambalo serikali bado hailitilii manani. (video na BBC)
No comments:
Post a Comment