HITMAKER wa Ngoma za Nibebe na Kwa Raha, Isihaka Nassoro ‘Aslay’, amesema kuwa kutokana na muziki kuwa sehemu ya maisha yake, amejikuta akiishi kama roboti kwa kufanya kazi mfululizo bila kupumzika.
Akipiga stori na Star Showbiz, Aslay aliyewahi kutamba na Yamoto Band akiwa na Marombosso, Becka Flavour pamoja na Enock Bella alisema, anaamini muda wa kupumzika kwa mwanadamu ni pale anapoondoka duniani, kwa hiyo kila siku yupo studio, kama siyo studio yupo lokesheni anafanya video na kama siyo lokesheni basi yupo kwenye shoo majukwaani.
“Sina muda wa kupumzika, kwa maana ninaamini mtu kupumzika ni pale anapofariki dunia, nafanya kazi kila siku ili kuhakikisha nasonga mbele kwenye maisha yangu,” alisema Aslay.
No comments:
Post a Comment