Rais wa zamani wa chama cha upinzani cha FDC Uganda, Dr Kizza Besigye na viongozi wengine wa upinzani nchini humo wamelaani mauaji ya Mbunge wa Manispaa ya Arua, Ibrahim Abiriga.
Jeshi la polisi na bunge mapema walisema kuwa Abiriga (wa chama cha NRM) pamoja na mlinzi wake waliuwawa karibu na nyumbani kwake huko Kawanda katika wilaya ya Wakiso jana jioni.
Watu walioshuhudia tukio hilo wamesema washambuliaji hao walikuwa wanatumia usafiri wa pikipiki.
Pamoja na kuwa Abiriga alikuwa upande ulioanzisha mjadala juu ya suala lenye utata la ukomo wa umri, viongozi wa upinzani akiwemo Dr Besigye, rais wa chama cha DP Norbert Mao, Erias Lukwago, Dr Abed Bwanika wamejitokeza kulaani mauaji hayo.
Akieleza wasiwasi wake juu ya mauaji haya, Dr Besigye alituma ujumbe wa tweet akielezea tukio hilo kama ni janga na kuongeza kuwa hali ya kutokuwepo usalama Uganda sasa imefikia kiwango cha kumuathiri kila mtu.
No comments:
Post a Comment