Mama mwenye Watoto watatu raia wa Kenya amefariki baada ya kufanya upasuaji wa kuongeza ukubwa wa matiti katika kliniki ya Nairobi.
Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa mama huyo wamesema kuwa ndugu yao alianza kusikia maumivu makali baada ya kutoka kufanyiwa upasuaji wa kuongeza matiti ikawabidi wampeleke katika hospitali ya Nairobi ili kupata matibabu.
Uchunguzi wa Madaktari uligundua kuwa upasuaji aliofanyiwa Mama huyo ulimsababishia madhara kwenye mwili wake kwani sehemu ya utumbo wa Mama huyo ulikatwa wakati wa upasuaji na kusababisha baadhi ya vitu kuvuja kitu kilichopelekea kuondoa uhai wake June 7.
Mama huyo ameacha Watoto watatu na mwili wake unategemewa kupumzishwa Juni 16 huko Kenya.
No comments:
Post a Comment