HABARI BURUDANI MICHEZO UDAKU AJIRA MUZIKI NA MENGINE MENGI KWENYE UKURASA HUU

  • Breaking News

    Friday, April 20, 2018

    NDUGAI: USALAMA WA BUNGE NI TOFAUTI NA WA DODOMA



    Dodoma. Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema licha ya kauli yake kuwa Mkoa wa Dodoma ni salama, haina maana hali ya usalama ilegezwe kila mahali ikiwamo Bungeni.
    Alisema hayo jana alipohojiwa kuhusu kauli aliyotoa bungeni juzi kuwa, moja ya sababu ya bunge kutohusisha mikataba ya watumishi wanne waliokuwa wanafanya kazi ofisi ya kambi ya upinzani na wengine ya CCM bungeni, ni kiusalama.
    ‘Yani Dodoma ikiwa salama basi ndiyo usalama ulegezwe kila mahali, aah! Bwana,” alisema Ndugai alipozungumza na gazeti hili mjini Dodoma. Aprili 5, akihojiwa na kituo cha terevisheni cha Azam ikiwa ni siku moja tangu aliporejea nchini akitokea India kwa matibabu, Ndugai alisema hali ya ulinzi Dodoma ni kubwa.
    Juzi akijibumwongozo wa Mbunge wa Ukonga (Chadema), Mwita Waitara kuhuu watumishi hao, Ndugai alisema sababu za kuwaondoa hao, mojawaponikiwa ni suala la kiusalama.
    Alisema watumishi waliokuwa wakipelekwa na vyama vya siasa walikuwa wanalipa ugumu Bunge, ikiwamo suala la usalama.
    Katika ufafanuzi wake jana Spika alisema, “ kwa watu wote ambao si watumishi wa Bunge kuwa wanaingia free katika jingo la utawala wa Bunge si sawa na huo ndiyo usalama wenyewe.
    “Siyo kama niwabaya , hatumaanishi kuwa wao ni watu hatari. Ndiyo maana tumewatoa na wa CCM. Tumeona tuwaondoe kwanza ili tuangalie upya.”
    Alipoulizwa iweje watumishi hao waibue hofu ya usalama wakati wanapendekezwa na vyama vya siasa vilivyopo Bungeni alisema, “Kwani vyama vitalipangia Bunge. Bunge lazima lijitengenezee mambo yake kwa kuwa chama Fulani kimemuamini mtu, basi. Wewe unaliona lipo sawasaw!” “Hata ninyi waandishi wa habari mko bungeni likitokea tatizo hata ninyi mnaweza kupata tatizo.”
    Alipoulizwa kuwa watumishi hao walikuwapo, alisema kila wakati lazima masuala mbalimbali yatazamwe upya.
    Kauli ya wabunge
    Mbunge wa Babati Vijijini (CCM), Jitu Vrajlal Soni akizungumzia suala hilo alisema uwapo wa watumishi hao ni msaada mkubwa kwa wabunge na kwamba, kama hoja ni usalama itazamwe upya.
    Alisema licha ya kutokuwa na uwezo wa kuingilia uamuzi huo, lakini inawezekana na watumishi hao wakatengewa eneo lao maalumu la kufanyia kazi kama inaonekana hawapaswi kutumia jingo la utawala.
    “Mimi ni mhasibu wa wabunge wa CCM hata sisi tumeathirika, lakini kwakweli suala linalotajwa ni usalama naomba liangaliwe upya. Mimi inanilazimu kwenda ofisi za CCM makao Makuu kila wakati kwaajili ya kufuata msaada wa vijana hao (watumishi),” alisema.
    Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari alisema hoja yausalama haina mashiko kwa maelezo kuwa Bunge lina uwezo mkubwa wa kudhibiti usalama.
    “Kila siku Bungeni wanaingia watu wengi ambao hukaguliwa ikiwamo wabunge wenyewe, iweje kwa watu wachache (watumishi) kushindwa kuthibitiwa kama wana hofu ya usalama,” alihoji.

    No comments:

    Loading...

    AJIRA

    SIMU

    AFYA

    UDAKU