HABARI BURUDANI MICHEZO UDAKU AJIRA MUZIKI NA MENGINE MENGI KWENYE UKURASA HUU

  • Breaking News

    Friday, April 20, 2018

    PICHA: Mwili wa Agnes Masogange wapelekwa Muhimbili


    Mwili wa Agnes Masogange wapelekwa Muhimbili
    Mwili wa aliyekuwa Video Vixen Agnes Gerald (Masogange) tayari umetolewa katika Hospitali ya Mama Ngoma na kupelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
    Mwanamitindo na video queen marufu bongo Agnes Gerald maarufu kama Masogange, amefariki dunia leo kwa tatizo la nimonia na kupundukiwa damu

    Akithibitisha taarifa ya kifo hicho muigizaji mkongwe Steve Nyerere amesema kwamba Agnes amefariki muda mfupi huu akiwa hospitali ya mama Ngoma Mwenge, na hivi sasa wanapeleka mwili hospitali ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.
    Agnes Masogange alikuwa maarufu baada ya kuonekana kwenye video kadhaa za bongo ikiwemo Masogange ya Belle 9.
    Video Queen’ maarufu nchini Tanzania, Agness Gerald maarufu kama Masogange amefariki dunia jioni ya leo Aprili 20, 2018 katika hospitali ya Mama Ngoma iliyopo Mwenge, jijini Dar es salaam.


    Akithibitisha taarifa hizo ndugu wa karibu na marehemu, Dick Sound amesema mwili wa marehemu unasafirishwa jioni hii kwenda kuhifadhiwa mochwari katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
    Wiki tatu zilizopita Masogange alishindwa kuhudhuria Mahakamani kusikiliza kesi iliyokuwa ikimkabili kwa kulazwa hospitalini kabla ya kesi hiyo kutolewa hukumu wiki iliyopita.
    Wanasiasa na Mastaa mbalimbali wa muziki na waigizaji wa filamu wametoa pole kufuatia taarifa hizo za mshtuko za kifo hicho, na Bongo5 inatoa pole kwa familia yake katika kipindi hiki kigumu.











    No comments:

    Loading...

    AJIRA

    SIMU

    AFYA

    UDAKU