Klabu ya soka ya Yanga imefanikiwa kufuzu katika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho barani Afrika licha ya kuambulia kichapo kutoka kwa wapinzania wao Welayta Dicha kutoka Ethiopia.
Katika mchezo huo wa pili ambao umechezwa katika uwanja wa Hawassa nchini humo, wenyeji wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 ambalo lilifungwa na Eshetu Mena dakika ya pili ya mchezo huo.
Matokeo hayo yanaifanya Yanga kusonga mbele kwa jumla ya ushindi wa mabao 2-1 kutokana na ushindi wa 2-0 iliyoupata katika mchezo wa kwanza uliochezwa wiki moja iliyopita katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha Yanga kilichoanza kwenye mchezo wa leo ni Rostand, Kessy, Mwinyi, Shaibu, Yondani, Kamusoko, Tshishimbi, Mhilu, Buswita, Raphael na Chirwa.
Wachezaji wa akiba: Benno Kakolanya, Juma Abdul, Gadiel Michael, Nadri Haroub, Said Ali, Juma Mahadhi na Emmanuel Joseph.
No comments:
Post a Comment