HABARI BURUDANI MICHEZO UDAKU AJIRA MUZIKI NA MENGINE MENGI KWENYE UKURASA HUU

  • Breaking News

    Friday, April 27, 2018

    VIDONDA VYA TUMBO (PEPTIC ULCER)



    VIDONDA vya tumbo, ni vidonda vidogovidogo vinavyotokea kwenye kuta za ndani za tumbo na sehemu ya juu ya utumbo mwembamba (duodenum) na husababisha maumivu makali ya tumbo kwa mhusika.


    CHANZO CHA TATIZO

    Vidonda vya tumbo husababishwa na bakteria waitwao Helicobacter pylori. Bakteria hawa huishi kwenye kuta za utumbo na hutengeneza vimeng’enya viitwavyo ‘Urease’ vinayopunguza athari za asidi ya asili iliyopo kwenye utumbo.
    Hali hii ikitokea, mwili nao hujitahidi kuzalisha asidi nyingi ili kufidia upungufu uliosababishwa na bakteria hawa na hapo ndipo tatizo linapoanza kwani asidi inayozalishwa hukwangua kuta za tumbo na kusababisha vidonda.
    Pia matumizi ya muda mrefu ya dawa za Asprin na za kutuliza maumivu kama Diclofenac, ibuprofen, Naproxen Sodium huchangia tatizo hilo. Pia tatizo hili huweza kusababishwa na kurithi, matumizi ya pombe na uvutaji wa sigara.
    Kuwa na msongo wa mawazo na kula vyakula vyenye viungo vingi, huongeza hatari ya mtu kupata ugonjwa huu au kama tayari mgonjwa ana vidonda vya tumbo, hali hizi husababisha tatizo liwe kubwa zaidi.



    DALILI ZA VIDONDA VYA TUMBO
    -Maumivu ya tumbo na  maumivu haya huwa makali zaidi pale asidi inapopita juu ya vidonda. Maumivu yanaweza kuanzia kwenye kitovu na kupanda juu hadi katikati ya kifua na huongezeka unapokuwa njaa. Pia yanaweza kuwa makali wakati wa usiku.
    – Kushindwa kumeza vizuri chakula.
    – Chakula kukwama kama kinataka kurudi mdomoni.
    – Kujisikia vibaya baada ya kula.
    – Kupungua uzito.
    – Kukosa hamu ya kula.
    Dalili za hatari ni kama kutapika damu, kupata choo kikubwa cheusi au chenye damu nzito, kichefuchefu na kutapika.

    MATIBABU YA VIDONDA VYA TUMBO
    Kama vidonda vitakuwa vimesababishwa na bakteria, dawa za kuua na kuondoa bakteria hutumiwa. Kama vidonda vya tumbo vitakuwa vimesababishwa na dawa za kutuliza maumivu na mgonjwa hana maambukizi ya bakteria, atapewa dawa za tofauti ambazo kitaalamu huitwa Proton Pump Inhibitors ‘PPI’. Matibabu haya yanaweza kuchukua muda kabla ya kuanza kufanya kazi hivyo daktari anaweza kuongeza matibabu mengine kama vizuia asidi ‘Antiacids’ kwa ajili ya nafuu ya haraka

    No comments:

    Loading...

    AJIRA

    SIMU

    AFYA

    UDAKU