HABARI BURUDANI MICHEZO UDAKU AJIRA MUZIKI NA MENGINE MENGI KWENYE UKURASA HUU

  • Breaking News

    Thursday, May 3, 2018

    UEFA: Liverpool yatinga fainali kwa kichapo, nusra kiwakute cha Barca



    Liverpool wamefanikiwa kutinga hatua ya fainali ya michuano ya klabu bingwa Ulaya tangu mwaka 2005 ambapo walinyakuwa kombe hilo kwa kuifunga AC Milan kwa penati 3-2 baada ya kufungana magoli 3-3 katika dkika za kawaida.
    Liverpool wamefanikiwa kutinga tena katika hatua hiyo usiku wa jana baada ya kuifunga AS Roma kwa jumla ya mabao 6-7 ingawa walifungwa kwenye mechi hiyo ya nusu fainali ya pili.
    Katika mchezo huo Roma walifanikiwa kushinda mabao 4-2. Mabao hayo ya Roma yalifungwa na James Milner aliyejifunga dakika ya 16, Edin Dzeko (52) na Radja Nainggolan aliyefunga mabao mawili (86 na 90).
    Nao Liverpool walipata mabao yao kupitia kwa Sadio Mane (9) na Georginio Wijnaldum (25).
    Liverpool watakutana na Real Madrid katika mchezo wa fainali ya michuano hiyo ambayo itafanyikamjini Kiev Mei 26 ya mwaka huu.

    No comments:

    Loading...

    AJIRA

    SIMU

    AFYA

    UDAKU