Mke wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva Alikiba, Aminah ameeleza kwa mara ya kwanza jinsi walivyokutana na mumewe hadi kufikia hatua ya kuoana.
Aminah amesema kwa mara ya kwanza walikutana kwenye Ndege na hakuwa anamfahamu vizuri lakini baadaye baada ya kupeana namba za simu alianza kuzoeana naye taratibu.
“Mara ya kwanza kukutana na ilikuwa kwenye ndege na hatukuzungumza mara ya pili Kaka yangu binamu ndiyo alinikutanisha nae maana walikuwa marafiki sana na hapo ndiyo tulianza urafiki wetu kabla ya kufika hapa tulipo,“amesema Bi. Aminah kwenye kipindi cha Leo Tena cha Clouds FM.
Hata hivyo, Bi. Aminah amesema kuwa Alikiba ndiye aliyeanza kumtamkia kuwa anampenda na yeye akamwambia kama ni kweli aende kwa wazazi wake akajitambulishe.
“Aliponitamkia anataka kunioa nikamwambia aje nyumbani kwa wazazi wangu na kweli akaja nyumbani kwa wazazi,”.amesema Bi. Aminah.
No comments:
Post a Comment