HABARI BURUDANI MICHEZO UDAKU AJIRA MUZIKI NA MENGINE MENGI KWENYE UKURASA HUU

  • Breaking News

    Friday, May 11, 2018

    Serikali yafuta leseni za madini

    Serikali imefuta leseni zote za kuhodhi maeneo ya madini na wamiliki wake wametakiwa kuomba upya wakizingatia Sheria ya Madini na kanuni zake.

    Mwenyekiti wa Tume ya Madini nchini, Profesa Idris Kikula, amesema, tangazo la Serikali namba moja la mwaka 2018 limesema maeneo yote yaliyopewa leseni yanarejeshwa serikalini bila hakikisho la kupewa tena.
     Amefafanua kuwa, uamuzi huo umefanyika kwa mujibu wa Sheria ya Madini ya mwaka 2010 ikisomwa na marekebisho yake ya mwaka 2017 na kanuni ya 21 ya kanuni za Madini (Haki Madini za mwaka huu).
     Amesema leseni zilizofutwa na wamiliki wake wanatakiwa kuomba tena zinazihusu kampuni 11, na kwamba leseni hizo zinajumuisha migodi ya kati na mikubwa.


    No comments:

    Loading...

    AJIRA

    SIMU

    AFYA

    UDAKU