Hatimaye hit maker wa Kwangwaru, Harmonize amefunguka kueleza kwamba yeye ni mmoja kati ya wamiliki wa Wasafi TV baada ya kukanusha kwa muda mrefu.
Muimbaji huyo alikuwa akikanusha suala hilo kila ambapo alipokuwa anaulizwa swali hilo, lakini Ijumaa hii amejikuta akilithibitisha suala hilo kupitia kituo cha redio cha Hot FM cha nchini Kenya.
Akiwa Hot FM ya nchini Kenya, Harmonize aliulizwa na mtangazaji juu ya kutoonyesha support ya kupromote kolabo yake na Willy Paul ndipo katika kujibu swali hilo akajikuta akieleza ishu ya umiliki wake wa Wasafi TV.
“Wakati yeye anapanga tarehe ya kurelease wimbo wake tulioshirikina, mimi nimesharelease Kwangwaru audio, nadhani baada ya wiki moja naye Eddy Kenzo akatoa wimbo wake ambao amenishirikisha, Willy akaniambia mimi nataka kutoa wimbo Monday nikamwambia oky, ikatengenezwa teaser ya Pilipili remix hata ukiingia kwenye Insta yangu ipo, na hata audio ilivyotoka nikapost video Insta huku nyuma ikisikika audio,” alisema Harmonize.
Aliongeza, “Lakini pia haikuishia hapo akanimbia kesho tuachie video, kwasababu mimi ni mmoja kati ya wamiliki wa Wasafi TV, nikaambia Wasafi kuna exclusive hii hapa, nyimbo ya Willy Paul amenishirikisha mimi inatakiwa kupata rotation sana. Pia kama nyimbo mpya inavyotoka kuna sehemu inawekwa kama exclusive ikawapa post ya tatu hiyo,”
Muimbaji huyo alikuwa nchini Kenya wiki hii kwaajili ya show yake ambapo pia alipata fursa ya kufanya media tour.
Kufutilia mahojiano yake yote angalia video hapo chini.
No comments:
Post a Comment