HABARI BURUDANI MICHEZO UDAKU AJIRA MUZIKI NA MENGINE MENGI KWENYE UKURASA HUU

  • Breaking News

    Wednesday, May 9, 2018

    JE NI KWELI RAISI HASHAURIKI: Bombadia moja "imekufa" Mwanza, ATCL inajigamba kuleta Dreamliner





    Hizi ni taarifa rasmi za wadau,kuwa ndege yetu moja ya bombadia,yenye usajili wa 5H-TCB imelala pale Mwanza.Sasa inaelekea mwezi mzima toka ndege hiyo imekubwa na hitilafu.Tatizo kubwa la kiufundi lipo kwenye injini moja.

    Wadau wanajadili kuwa tatizo kubwa la ndege hiyo ni injini moja kufa kabisa,na "mgogoro" upo ni kama gharama ziwe kwa shirika la ATCL au kwa "manufacturer".ATCL wanadhani kuwa manufacturer anapaswa kulipa,wakati manufacturer anaamini shirika ndilo linawajibika na tatizo hilo.Haya ni majanga yanayoikumba ATCL.Na sasa bombadia yetu imelala pale Mwanza ikisubiri "mgogoro huu wa kiuwajibikaji" utatuliwe.Bunge lilipaswa kuuliza,hii ni ndege ya shirika la umma,shirika ambalo kwa sasa pesa za kodi zetu zimetumbukizwa kuliko mashirika mengine yote.Ni halali yetu kujua tatizo ni nini??


    Wakati tukiwa hatuna hata wataalamu wa kutosha wa kuhudumia ndege za bombardier kwa maana ya wahandisi wazalendo,tayari serikali imeagiza ndege za makabila mawili tofauti,yaani CS300 na Dreamliner.Ni ukweli kuwa hata wahandisi waliobobea tunaowategemea katika shirika letu kwa sasa ili kuhudumia bombadia zetu ni kutoka Ethiopia,Misri na Malawi.Hawa wanalipwa na serikali yetu,hawa vijana wazalendo ndio tunaendelea kuwasomesha na kuwaongezea ujuzi ili wapate leseni hata za kuzisimamia bombardia zetu

    Ni ama wasaidizi wa Rais hawafikishi ushauri toka kwa wataalamu,au washauri wanashindwa kuufikisha ukweli kama ulivyo,au wapokea ushauri hawapo tayari kupokea wanavyoshauriwa.Ushauri mwingi umepelekwa kwa njia rasmi kwa wahusika,lakini watu wanataka sifa za kisiasa na kuona ahadi zinafikiwa wakati hakuna tija (Productivity), kuwa "kachumbari" hii inayotaka kufanywa na ATCL kwa sasa haina afya kiuchumi na kiutendaji (Operational).

    Kuhudumia ndege za makabila matatu tofauti katika shirika moja ni kukaribisha kabuli na kifo cha kiuchumi.Hii ATCL yenyewe huko Mumbai inakotaka kwenda tiketi zake zitauzwa na "dalali" tu maana mpaka sasa imeshakuwa "black-listed" na IATA, hivyo kuondolewa katika mfumo rasmi wa kibiashara na unaoaminika wa ukataji wa tiketi unaounganisha mashirika yote duniani.Huyo dalali hawezi kufanya kazi bila faida,lazima atupige.

    Ukweli wa deni hili lililokubuhu la ATCL,sio siri tena,maana ingekuwa ni siri basi serikali isingesikiliza ushauri wa wadau kuwa ndege hizi mpya izipachike kwa TANZANIA GOVT FLIGHT AGENCY, maana zingetamkwa tu kuwa ni mali ya ATCL, hakuna hata moja ambayo ingesalia. Wenye kutudai wangezipokonya zote. Ukweli huu usemwe pia kuwa hizo safari za Mumbai tiketi anakata nani na sisi hatumo kwenye mfumo wa IATA? Maana mfumo wa IATA unasaidia unapokuwa China,India au Ulaya, unakata tiketi ya kufika Dsm-Tanzania, itakutolea orodha ya mashirika yanayofika Dsm Tz,sababu sisi hatupo IATA, hiyo ya Mumbai dalali wetu ni nani??

    Sisi wengine tuliiopongeza "idea" ya kununua ndege aina ya bombadia tukiwa na matumaini ya kuanza kwanza na "local routes", tukisimama tuhamie kwenye "regional routes" na tuki-settle mambo yetu na IATA tuhamie kwenye "international routes". Ndio maana kwa wanaokumbuka mwanzoni Rais alikuwa analitangazia Taifa kuwa atanunua ndege aina ya Airbus,ila tulipenyeza ushauri wetu na akatusikia,akaachana na Airbus nakununua hizi bombadia. Na sasa atusikie kupitia JF maana kwa njia rasmi naona wasaidizi wake hawamfikishii.

    Bombadia na Dreamliner ni machine mbili tofauti sana sana,jumlisha hii CS300,kuhudumia machine hizi tatu katika shirika moja ni kudanganyana.Tusijitafutie hasara za kujitakia.Biashara ya ndege haiitaji siasa.

    Halafu, hao wanaoifuata hii Dreamliner watuambie ukweli, unaweza kweli kupata dreamliner mpya kwa order ya miaka miwili tu? Yaani ukae miaka miwili na utengenezewe dreamliner mpyaaa wewe mteja wa ndege moja, wakati kuna wenye order za ndege 100 bado wako kwenye foleni? Tuangalie tusije tukapewa zile "reject" za majaribio,na kwa kuona tumekubali hata "reject" wakaamua kutupoza na moja ya "nyongeza", maana nimeona kuna clip Rais anasema tulipoagiza hiyo moja, wameamua kutupa na moja ya "nyongeza".

    Bora haya mambo tuyaseme mapema,ili tusije tukapeana lawama huko mbele ya safari,maana mzee mwenyewe anasema, msema kweli ni mpenzi wa Mungu. This "haterogenious fleet" is going to kill our dreams

    Mashirika mengi duniani na hasa yanayotaka kuinuka kurudi ktk ushindani wa soko la usafiri wa anga,huwa wana kitu wanaita "Fleet Commonality"; yaani shirika la ndege linaamua kununua au kukodisha ndege za jamii moja, zinazotoka kwa manufacturer mmoja lkn zikawa na model pamoja na generation tofauti.

    Yaani mnaamua kama ni kuwa ni Airbus,basi shirika linakuwa na ndege zote toka Airbus lkn zikatofautina model na generation, au mkatumia Boeing, Bombardier, ATR, Embraer n.k bila kuwa na mchangayiko

    Hii "Fleet Communality" ina aina nyingi;inaweza kuwa "same model and Same Generation" ya ndege, mfano Boeing 737-700, B737-700ER na B737-700c au "Same model" na "different Generation", mfano Boeing 737-700 New Genaration au MAX737 nk.

    Na kuna mashirika ambayo huwa yanataka kurudi katika sekta ya usafiri wa anga,ile just for prestige,haya huwa hayaangalii faida bali ile "prestige" tu ya Taifa, kwamba nchi hii ina ndege au nchi hii shirika lake linazunguka nchi kadhaa za Afrika, Ulaya au Amerika. Falsafa ya mtaji wa mashirika kama haya, huwa sio faida, bali namna nyingine ya kuitangaza nchi na kujitutumua katika ulimwengu wa kisiasa.

    Nchi kama hizi huwa hazioni shida kupata hasara,wanawekeza mtaji mkubwa katika ndege lakini hakuna faida wanayoipata zaidi ya hasara na prestige. Hii ndiyo anaifanya jirani yetu wa maziwa makuu. Hajali sana juu faida itokanayo na shirika,bali "prestige" ya nembo la Taifa lake popote inapeperuka ndege yake ikiwa na bendera ya Taifa lake.

    Rais JPM kwa mara moja amenunua ndege aina ya Bombardier Dash8-Q400(Next Generation),na sasa ametoa ahadi ya kuleta ndege nyingine aina ya Bombardier CS300.Ndege hizi zote ni "Kabila" moja la Bombardier lkn ni "ukoo" tofauti,moja ni turboprop engines wakati mwingine ni jet engines.

    Tujifunze kwa LAM(Mozambique) walioamua kuwa na Boeing na E190, Kenya walioamua kuwa na Boieng na E190,Ethiopia walioamua kuwa na Boeing na Bombardier,South Africa Airways walioamua kuwa na Airbus na Boeing,Egypt Air walioamua kuwa na Boeing na Airbus. Hii "kachumbari" ya Pangaboi,CS300 na Dreamliner, inaweza kuturudisha kulekule tulipojikwaa.

    Kununua tu hiyo "Flight Simulator" ya Dreamliner kwa ajili ya kufundishia marubani ni sawasawa na kununua bombardier nyingine.Mwisho wa siku,hizo ndege zikija,na kwa kiwango cha kimataifa cha kuzihudumia,tutakodisha kuanzia rubani mpaka injinia wa dreamliner sbb kuwapata wazawa itachukua muda mrefu kidogo.Wakati tunataka kurirudisha shirika angani,basi tungefuata "Fleet Commonality" ili baadae ndio tuingie kwenye hiyo "Cross Manufacturing".

    Ni mtazamo tu, hatuisimangi ATCL,wala hatuna haja ya kuwakatalia watu kutimiza ahadi zao za majukwaa ya kisiasa, lakini palipo na ukweli basi siasa ikae kando na tuuishi uhalisia.


    chanzo: jamiiforums

    Inawezekana Rais hashauriki au hafikishiwi ushauri; Bombadia moja "imekufa" Mwanza, ATCL inajigamba kuleta Dreamliner


    No comments:

    Loading...

    AJIRA

    SIMU

    AFYA

    UDAKU