HABARI BURUDANI MICHEZO UDAKU AJIRA MUZIKI NA MENGINE MENGI KWENYE UKURASA HUU

  • Breaking News

    Tuesday, May 8, 2018

    Zambia: Wanafunzi wa kike waonywa kutovaa nusu utupu kwenye maktaba chuoni

    Moja kati ya vyuo vikuu vya juu nchini Zambia kimewaonya wanafunzi wa kike kutoingia maktaba wakiwa ''nusu utupu''kwa sababu vitendo hivyo vinawafanya wanafunzi wenzao wa kiume kutokuwa makini.
    Chuo kikuu cha Zambia kimeweka matangazo kwenye maeneo ya maktaba kikiwataka wanafunzi wa kike kuvaa vizuri.
    ''Tumebaini kuwa baadhi ya wanafunzi wa kike wanavaa nusu utupu wakiwa maktaba, hali inayosumbua wanafunzi wa kiume.'' lilieleza tangazo hilo
    ''Hivyo tunawashauti wanafunzi wa kike kuvaa vizuri wanapokuwa kwenye maeneo ya chuo.
    Baadhi ya wanafunzi wa kike hawakubaliani na amri hiyo
    ''Kama nia yako ni kwenda maktaba kusoma, kwanini uanze kuangalia vitu vingine kama miguu ya wasichana?'' Mwanafunzi wa mwaka wa tatu Dikina Muzeya ameiambia BBC.
    ''Zingatia vitabu vyako, basi.''


    Lakini Killion Phiri, mwanafunzi wa kiume anakubaliana na uamuzi wa mamlaka.
    ''Unajua jinsi miili ya wanawake inavyovutia.Utawezaje kuzingatia kusoma wakati mtu anaingia amevaa sketi fupi au nguo ya kubana.Utaanza kufikiria kuhusu vitu vingine na hautaweza kuwa makini.

    No comments:

    Loading...

    AJIRA

    SIMU

    AFYA

    UDAKU