Habari zilizoenea ni kwamba Jet Li, mcheza karate maarufu na ambaye amewahi kucheza sinema kama Romeo Must Die, The expendables, Kiss of the Dragon, nk, hali yake ya afya sio nzuri.
Jet Li, mwenye umri wa miaka 55 kwa sasa, anasumbuliwa na ugonjwa wa "hyperthyroidism" ambao humfanya mtu kujisikia kuchoka na kupungua uzito.
Hii kwa uhakika ni habari yenye kusikitisha kwa wapenzi wengi wa film za Jet Li, ambaye hajacheza sinema yoyote kubwa kwa muda wa miaka 10 iliyopita. Jet Li mwenyewe amekuwa akisema kwamba "nasikia maumivu, lakini siteseki na nina furaha" kutokana na huu ugonjwa.
Hata hivyo inasemekana Jet LI yuko katika mazungumzo ya kucheza sinema itakayoitwa "Mulan" kama emperor wa China. Sinema hii inatarajiwa kutolewa mwaka 2020.
No comments:
Post a Comment