Mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) unakila dalili za uwezekano wa kusambaa, Shirika la Afya Duniani (WHO) limetahadharisha Jumatano, wakati ikiripoti vifo saba zaidi vilivotokana na ugonjwa huo.
“Tuko katika shambulizi la maradhi hatari yanayoenea kwa kasi,” Peter Salama, mkuu wa utoaji huduma za dharura, WHO, ameuambia mkutano maalum juu ya mlipuko ambao tayari umeuwa watu 27.
“Katika wiki chache zijazo tutafahamu iwapo mlipuko huu utaenea kaitka upande wa mjini au tutaweza kuudhibiti, amesema Salama.
Shirika hilo limetoa idadi mpya ya vifo, ikieleza kuwa kulikuwa na wagonjwa 58 wa Ebola tangu mlipuko huo kutangazwa Mei 8 – ongezeko la idadi ya watu saba juu ya ile iliyotolewa Jumanne - - na kusema kuwa inachukua hatua kuwafuatilia zaidi ya watu 600 waliokuwa wamegusana au kuwakaribia wagonjwa hao.
Ikiwa ni moja ya maradhi yanayotisha zaidi duniani, Ebola ni kirusi kinacho sababisha homa ya kutoka damu ambayo husambaa kupitia kugusa majimaji ya mwilini mwa mgonjwa na unaweza kupelekea viungo vya ndani ya mwili kutoka damu kwa wingi, pia mdomoni, machoni na masikioni.
Mlipuko wa ugonjwa huo ulianza katika kijiji kilichoko kaskazini magharibi mwa DRC katika eneo lilioko nje kabisa linaloitwa Bikoro.
Alhamisi iliyopita, mgonjwa wa kwanza aliripotiwa huko Mbandaka – mji wenye watu takriban bilioni 1.2 ambao uko pembezoni mwa mto Congo, ambao ni kituo kikuu cha usafiri kwenda upande wa chini wa mto huo huko Brazzaville na Kinshasa na upande wa juu ya mto huo kuelekea Bangui.
No comments:
Post a Comment