Mshambuliaji wa klabu ya Everton, Wayne Rooney anatarajiwa kuwasili Washington siku ya Alhamisi kwaajili ya mazungumzo pamoja na kufanya vipimo vya afya katika klabu ya DC United inayoshiriki ligi ya Marekani (MLS).
Msemaji wa Rooney amethibitisha kuwa nahodha huyo wazamani wa timu ya taifa ya Uingereza atakwenda Marekani na wakala wake, Paul Stretford ili kufanya mazungumzo ya mwisho na Mkurugenzi wa DC United, Jason Levien na Meneja Mkuu, Dave Kasper.
Dili hilo ambalo bado halijakamilika litashuhudia, Rooney akiondoka Goodison Park kwa dau la pauni milioni 12.5 litakalo mfanya kusalia hapo mpaka msimu wa mwaka 2020.
No comments:
Post a Comment