HABARI BURUDANI MICHEZO UDAKU AJIRA MUZIKI NA MENGINE MENGI KWENYE UKURASA HUU

  • Breaking News

    Monday, May 21, 2018

    Kenya yachukua tahadhari dhidi ya homa ya Rift Valley



    Serikali ya Kenya imetoa tahadhari Jumatatu juu ya uwezekano wa kuwepo mlipuko wa homa hatari ya Rift Valley inayouwa mifugo wakati mvua zikiendelea kunyesha kwa wingi.
    Kutokana na tishio hili wafugaji, wafanyakazi wa machinjioni, wakulima na madaktari wa mifugo wametahadharishwa katika kiwango cha juu, juu ya uwezekano wa maambukizo ya mifugo inaweza kuwaathiri wanadamu iwapo watagusa damu au sehemu mbalimbali za miili ya wanyama waliokuwa na maradhi hayo.
    Tamko lililotolewa na Wizara za Afya na Kilimo zimetaja wananchi katika nchi 17 zilizokuwa na uwezekano mkubwa wa kukumbwa na mafuriko ikiwemo Mombasa, Baringo na Nairobi kwamba ziko katika hatari kubwa zaidi.
    Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Huduma za Mifugo, Dkt Obadiah Njagi na mwenza wake katika huduma za afya Dkt Kioko Jackson, hakuna ugonjwa unaotokana na maambukizo ya wanyama uliogunduliwa kutoka katika mifugo au binadamu.
    “Mlipuko mkubwa wa mwisho ulikuwa mwaka 2006/2007 baada ya kumalizika mvua za El Nino ambapo kulitokea takriban vifo 160 vya wanadamu na hasara ya shilingi bilioni 4 katika secta ya mifugo,” wamesema.

    No comments:

    Loading...

    AJIRA

    SIMU

    AFYA

    UDAKU