Msanii wa muziki kutokea nchini Nigeria, Davido kwa mara nyingine tena amefunguka kuhusu mipango ya kufanya kolabo na Alikiba.
Muimbaji huyo katika mahojiano na Clouds FM katika kipindi cha Bongo Fleva amesema bado hawajafanya kolabo ila ikitokea ni kitu ambacho kitafanyika.
Muimbaji huyo katika mahojiano na Clouds FM katika kipindi cha Bongo Fleva amesema bado hawajafanya kolabo ila ikitokea ni kitu ambacho kitafanyika.
“Bado sijafanya kolabo na Alikiba ila tayari tushakutana kwenye show kama mbili hivi na ikitokea akija na kutaka kufanya kolabo na mimi basi tutafanya” amesema Davido.
Ameongeza kuwa hata wasanii wa Tanzania wakimfuata kwa mazungumza kwa lengo la kutaka kufanya naye kazi yeye yupo tayari.
Jibu la Davido halina tofauti na lile alilotoa Alikiba July 2017 kuhusu kolabo yao. Alikiba alisema; ‘Unajua wasanii muda mwingine tunakuwa na maneno ya kuridhisha watu lakini hakijafanyika chochote ila plan zipo, muda tukiupata tutafanya ila sijajua ni lini,’.
No comments:
Post a Comment