Klabu ya Leeds United imethibitisha kuingia kandarasi ya miaka miwili na Muargentina, Marcelo Bielsa ya kuifundisha timu hiyo.
Klabu hiyo imekuwa kwenye harakati za kutafuta kocha mpya atakaye weza kurithi mikoba ya Paul Heckingbottom aliyetimuliwa kazi tangu tarehe moja ya mwezi Juni baada ya kuiyongoza timu hiyo kwa muda wa miezi minne ndani ya Elland Road.
Muargentina huyo amewahi kufundisha timu ya Chile pamoja na klabu nyingi za barani Ulaya kama Athletic Bilbao, Marseille na Lazio.
No comments:
Post a Comment