HABARI BURUDANI MICHEZO UDAKU AJIRA MUZIKI NA MENGINE MENGI KWENYE UKURASA HUU

  • Breaking News

    Friday, June 15, 2018

    POLISI "WAUA" MWINGINE ASIYE NA HATIA MKOANI MBEYA.



    Jeshi la polisi mkoani Mbeya linadaiwa kumuua kwa kipigo kijana Frank Kapange, mwenye umri wa miaka 21, mkazi wa Ilonga Mwambene jijini Mbeya. Frank anadaiwa kupigwa na kari polisi waliokuwa doria, na kiasi cha kuharibiwa ini lake na hivyo kufariki muda mfupi baada ya kufikishwa hospitali.
    Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Gideon Siame inaeleza kuwa tukio hilo la kusikitisha lilitokea jijini Mbeya, usiku wa kuamkia tarehe 05/06/2018. Baba mdogo wa kijana huyo amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kwamba kinachoendelea kwa sasa ni uchunguzi wa mwili wa marehemu, pamoja na kubaini askari waliohusika ili waweze kuchukuliwa hatua.
    Hata hivyo ndugu hao wamezira kuzika mpaka taarifa ya uchunguzi itakapotolewa. Mwili wa Frank umehifadhiwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Mbeya. Kamanda wa polisi wa mkoa wa Mbeya alipotafutwa kwa simu kuelezea juu ya tukio hilo, simu yake iliita tu pasipo kupokelewa.
    Mama mzazi wa Frank ameelezea kwa masikitiko kkifo cha kijana wake anayedaiwa kuuawa kinyama na jeshi la polisi, akisema Frank ndiye aliyekuwa akitunza familia na wadogo zake, kwani baba yao alishafariki. Msiba upo nyumbani kwa marehemu kata ya Ilomba Mwambene nyuma ya kanisa la Roma.!

    No comments:

    Loading...

    AJIRA

    SIMU

    AFYA

    UDAKU