HABARI BURUDANI MICHEZO UDAKU AJIRA MUZIKI NA MENGINE MENGI KWENYE UKURASA HUU

  • Breaking News

    Friday, June 15, 2018

    Ni vita kali baina ya Misri dhidi ya Uruguay kombe la Dunia Urusi

    Baada ya mwenyeji timu ya taifa ya Urusi kuibuka na ushindi mnono wa jumla ya mabao 5 – 0 dhidi ya Saudi Arabia hapo jan, hii leo michuano hiyo ya kombe la dunia itaendelea kwa viwanja kadhaa kuwaka moto.

    Mafarao wa Misiri watakuwa na kibarua kizito cha kuwakabili Uruguay mchezo unaotarajiwa kuanza kupigwa majira ya saa 9:00 alasiri kwenye Uwanja wa Ekaterinburg.
    Nyota wa Misri, Mohamed Salah anapewa nafasi kubwa ya kuwemo kwenye kikosi cha mafarao hao baada ya kukosekana kwa muda tangu kupata majeraha kwenye mchezo wa fainali ya michuano ya klabu bingwa barani Ulaya wakati akiitumikia klabu yake ya Liverpool ilipoikabili Real Madrid.
    Mchezo mwingine ni baina ya timu ya taifa ya Morocco ikishuka kwenye dimba la St. Petersburg na kuikabili Iran .

    No comments:

    Loading...

    AJIRA

    SIMU

    AFYA

    UDAKU