HABARI BURUDANI MICHEZO UDAKU AJIRA MUZIKI NA MENGINE MENGI KWENYE UKURASA HUU

  • Breaking News

    Monday, June 11, 2018

    Penzi la Zari na Diamond ndio basi tena



    Baby Mama wa Diamond Platnumz, Zari The Boss Lady ameweka wazi kile kinachoendelea kati ya mzazi mwenzie baada ya kuwepo taarifa kuwa wamerudiana.

    Mrembo huyo ameeleza kilichopo kwa sasa ni makubaliano kuwa watashirikiana kama wazazi katika kulea watoto wao na si vinginevyo. Kupitia mtandao wa SnapChart ameandika;
    Just to clear the air, we are not back together but have agreed on co-parenting as per my break up post that we will remain great parents to our lovely kids. Just a lil note to all our fans. We love you too.
    Hii si taarifa nzuri kwa wale mashabiki waliokuwa wakivutia na couple hii kwa kipindi kirefu na kutamani kuiona tena.
    Utakumbuka hivi karibuni meneja wa Diamond, Babu Tale alienda Afrika Kusinia ambapo anaishi Zari ili kusuluhisha tofauti za wawili hao. Hakuna yeyote kati yao aliyetoa jibu la uhakikika iwapo mahusiano hayo yamerudi zaidi ya hiki alichoeleza Zari leo.
    Katika mahusiano yao Zari na Diamond walijaliwa kupata watoto wawili ambao ni Tiffah na Nillan. Zari ndiye aliyetangaza kuvunja mahusiano na Diamond kwa kile alichodai muimbaji huyo alikuwa akimvunjia utu wake kwenye mitandao

    No comments:

    Loading...

    AJIRA

    SIMU

    AFYA

    UDAKU