UKIE-NDA nchi ya Sierra Leone au Ghana ukaulizia maana ya jina la Koffi lazima utaambiwa ni Ijumaa. Katika mila nyingi za nchi za Magharibi mwa Afrika watoto wa kiume wana majina kulingana na siku waliozaliwa.Mfano mtoto wa kiume anayezaliwa Jumatatu anaitwa Kojo, wa Jumanne anaitwa Komla, Jumatano anaitwa Kwaku, Alhamisi ni Yao, Ijumaa ni Koffi, Jumamosi Kwame wakati Jumapili ni Kwasi.
Julai 13, 1956 katika mji wa Kisangani, Kaskazini mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), alizaliwa mkali wa Muziki wa Soukous (Lingala/Rumba ya Kongo), Koffi Olomide ukipenda waweza kumuita Grand Mopao, Numberi One, Mikael Jacksonee, Golden Star, Quadra Kora, Fololo Papa, Papa Happiness, Rapid Intervention Force, Golden Star, World No. 1, Quadra Kora Man, Mopao Mokonzi, MM, High Priest Mother, Nzambe Ya Ba Na Africa, Golden Ball, BB Taste, Favorite Dish na mengine mengi.
Ukiachana na historia hiyo fupi, Koffi pamoja na mkewe, Aliana wamebarikiwa kuwa na watoto saba, Nzau Twengi, Elvis, Minou, Rocky, Del pirlo Mourhino, James pamoja na Didi Stone.
Didi Stone
Didi ni miongoni mwa watoto wa Koffi ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 18, ni mmoja kati ya wabunifu wa mavazi wanaokuja kwa kasi nchini Ufaransa. Akifanyiwa mahojiano na jarida maarufu nchini Ufaransa la Vogue, Didi anasema aliyemvutia kujiingiza katika mitindo ni staa wa Muziki wa Pop, Rihanna.
“Nampenda sana Rihanna, kwa sababu huwa haogopi kujaribu vitu vipya mwilini mwake. Wakati mwingine naangalia wanamitindo kwenye majarida na kupenda wanavyojaribu ubunifu wa nywele lakini kwenye utofauti wa rangi. Napenda sana!”Kichwa chake Didi alianza kupata umaarufu kwenye ubunifu wa nywele za kichwani mwake ambapo amekuwa akizibadilisha kwa staili nyingi na muonekano tofauti.
“Natengeneza nywele zangu mwenyewe. Ni mwanamke ambaye namtengeneza pia nywele mama. Katika tamaduni zetu suala la nywele huchukua muda mrefu kutengeneza, nafanya hivyo nyumbani. Situmiii kemikali wala kibaya chochote. Naziosha mara moja kwa wiki, lakini mara nyingi natumia krimu au shampoo basi.”Kuhusu Koffi
Akifanyiwa mahojiano mbalimbali, Koffi alishawahi kukiri kuvutiwa na ubunifu wa Didi na kumpa nafasi ya kumbunia mavazi mbalimbali ambayo amekuwa akiyavaa pindi awapo jukwaani au matembezi. Hata Didi mwenyewe anaona fahari kumbunia baba yake.
“Najisikia furaha sana, watu wanakuona wewe ni wa tofauti, inakufanya uaminike,” anasema Didi kuhusu kumbunia baba yake huyo aliyewahi kubamba na kibao cha Selfie. Katika mavazi hayo, mengi yamekuwa gumzo kutokana na kwenda na fasheni lakini pia kuna ambayo yamemfiti japokuwa umri nao wa miaka 61 umemtupa mkono. Makala haya yanaanika mavazi hayo;
MAKALA: ANDREW CARLOS
No comments:
Post a Comment