Mhubiri mmoja wa Kiinjilisti nchini Marekani amedaiwa kuwaomba waumini wake kuchanga fedha za kumsaidia kununua ndege yake ya Nne.
Mhubiri huyo amedaiwa akisema kuwa hata kama Yesu angekuwepo siku hizi, "hangekuwa anapanda punda".
Jesse Duplantis amesema Mungu amemwambia anunue ndege aina ya Falcoln 7X ambayo inagharimu dola za Kimarekani milioni 54.
Ameongeza kuwa alikuwa na shaka pia kuhusu kuendelea na ununuzi huo mwanzoni, lakini Mungu alimwambia: "Sikukwambia uilipie. Nilikwambia uamini na utaipata."
Ingawa si jambo la kushangaza kwa wahubiri kumiliki ndege zao binafsi, ombi lake kwa waumini kuchangia limezua shutuma nyingi.
Watu kwenye Twitter wamepokea ombi hilo kwa mshangao na wengi kunukuu aya katika Biblia zinazotahadharisha dhidi ya ulafi na "manabii wa uongo".
Wengine wanasema fedha hizo zinazotumiwa kutumia ndege zingeweza kutumika vyema kuwasaidia maskini.
No comments:
Post a Comment