MUIGIZAJI wa kitambo Bongo Muvi, Chuchu Hans amefunguka kuwa watu wanaomhukumu kuwa anakosea kuwa karibu na mzazi mwenziye ambaye ni muigizaji pia, Vincent Kigosi ‘Ray’ wakati huu wa mfungo wa Ramadhani na yeye ni Muislamu waache kwani wao siyo Mungu.
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu akiwa nchini Afrika Kusini na mzazi mwenziye huyo kwa ajili ya kushuti filamu, alisema kuwa kuishi na mzazi mwenziye huyo kwa ajili ya kazi haoni kama ni dhambi lakini anashangaa watu wanavyotoa hukumu mitandaoni kwamba anakosea.
“Mimi ninachojua wa kumhukumu mtu ni Mungu pekee kwa sababu yeye ndiyo anajua ukweli wote na anajua kila kitu cha binadamu na si mtu mwingine, najua nilivyo huku na Ray watu wanasema sana tu lakini sijali,” alisema Chuchu
No comments:
Post a Comment