Tukio la aina yake limetokea usiku wa kuamkia ya Leo katika eneo la Rau Madukani manisapaa ya Moshi.Tukio hili limepelekea watu wengi kujazana nje ya nyumba ya wageni iitwayo #SELEEN Mara tuu baada ya tukio hili kujitokeza katika nyumba hiyo ya wageni inayotambulika kama machinjioni.
Hata hivyo taarifa kutoka kwa mhudumu wa guest ile aitwaye Mariamu anasema mwanaume marehemu ni mteja wa muda mrefu Ila baada ya askari kupitia vitabu vya taarifa za wageni waingiao na watokao(attendance), haikuonesha kwamba mwanaume yule ni mteja wa Guest ile kama alivyosema mhudumu yule.
Hata hivyo ilikuja kugundulika kwamba kila mwanaume yule alipokuwa akifika pale quest nakupenda kuandika jina lake halisi.Ndio kitambulisho chake cha uraia kilichokuwa katika wallet yake kilipofichua ukweli wa majina yake kamili.
Kumbe kila alipokuwa akifika pale guest hakujiandikisha kwa majina yasiyo sahihi na haikuweza kufahamika kwanini hakuwa mkweli katika kujiandikisha.
Hata hivyo kwa mujibu wa mhudumu yule ni kwamba mwanaume yule kila alipokuwa akija alikuja mwenyewe na kisha kutoka na kwenda mtaani muda wa SAA 2 usiku hadi SAA 3 na kurejea na mwanamke ambaye hushinda nae na kesho yake jioni ndio mwanamke hiyo huondoka.
Hata hivyo ukaguzi wa mazingira ya quest yameonesha mwanaume yule aliji-overdose dawa ya nguvu za kiume iitwayo #Erector ambapo yamekutwa mapakiti matatu ya 50mg ambayo ni jumla ya 150 mg ambayo ni kiwango kikubwa sana kwa mwanaume kukutumia kwa mkupuo.
Mwanaume hapaswi kutumia zaidi ya 100mg kwa wakati mmoja. Ikumbukwe dawa hizi hazipaswi kutumiwa na wagonjwa wenye historia ya magonjwa kama blood pressure na magonjwa ya moyo. Hii hupelekea vifo vya ghafula vya wagonjwa hao. Dawa hizi huongeza msukumo wa damu, yaani blood pressure na mapigo ya moyo.
Tuwe makini kabla ya kutumia dawa hizi.
Hata hivyo mwanamke aliekuwa nae ndani ya guest hakuweza kufahamika kwa kuwa alitoweka hadi wahudumu kushangaza mlango wa nyumba hiyo ya marehemu ukiwa wazi saa 12 asubuhi jambo ambalo halikuwa kawaida kwa kuwa yeye hulipia siku tatu nzima kila anapokuja.
Mwili wa marehemu umepelekwa kuhifadhiwa katika hospitali ya Mawenzi kwa uchunguzi zaidi na uchunguzi zaidi.
No comments:
Post a Comment