HABARI BURUDANI MICHEZO UDAKU AJIRA MUZIKI NA MENGINE MENGI KWENYE UKURASA HUU

  • Breaking News

    Monday, May 14, 2018

    Muigizaji Elizabeth Michael 'Lulu' abadilishiwa adhabu, sasa kutumikia kifungo cha nje



    Muigizaji wa filamu nchini Elizabeth Michael, maarufu Lulu, amebadilishiwa adhabu na sasa anatumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu Tanzania.

    Lulu alihukumiwa kifungo cha miaka miwili jela Novemba mwaka jana baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia msanii mwenzake, Steven Kanumba.

    Akizungumza na MCL Digital Jumatatu Mei 14,2018, Ofisa Habari wa Jeshi la Magereza, Lucas Mboje amesema Lulu amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo cha nje kwa amri ya Mahakama Kuu ya Tananzia, Dar es salaam.

    "Lulu amebadilishiwa adhabu na ameachiwa juzi Jumamosi kati ya saa 2 hadi 3 asubuhi. Hii si kwamba ameachiwa huu, bali amebadilishiwa adhabu na atatumikia kifungo cha nje, kitaalamu tunaita ' Community service' amesema Mboje

    Chanzo: Mwananchi 

    No comments:

    Loading...

    AJIRA

    SIMU

    AFYA

    UDAKU