HABARI BURUDANI MICHEZO UDAKU AJIRA MUZIKI NA MENGINE MENGI KWENYE UKURASA HUU

  • Breaking News

    Tuesday, May 29, 2018

    Nairobi, Kenya. Jeshi la Polisi limewakamata na kuwaweka ndani maofisa wa ngazi ya juu zaidi ya 50



    Nairobi, Kenya. Jeshi la Polisi limewakamata na kuwaweka ndani maofisa wa ngazi ya juu zaidi ya 50 na watendaji wakuu baada ya wananchi kuonyesha hasira kutokana na madai ya wizi wa zaidi ya dola za Marekani 100 milioni katika mashirika ya serikali.

    Baada ya zaidi ya wiki ya kusoma habari nyingi katika kurasa za mbele za magazeti ya Kenya na mitandao ya jamii, ofisi ya mwendesha mashtaka ya umma ilitangaza Jumatatu kwamba mashtaka yatafunguliwa kwa watuhumiwa wote ambao majina yao yatakuwa katika mafaili yaliyoandaliwa na idara ya uchunguzi wa makosa ya jinai.

    Watuhumiwa hao ni pamoja na Mkuu wa Shirika la Vijana wa Huduma kwa Taifa (NYS) Richard Ndubai, viongozi waandamizi na wanachama wanne wa familia moja, wanaohusika katika biashara ya ufisadi.

    Watuhumiwa hao kwanza walipelekwa kwenye vituo vya polisi vya Muthaiga, Gigiri na Makao makuu kisha wakapelekwa makao makuu ya Kurugenzi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kiambu Road, Nairobi.

    Rais Uhuru Kenyatta, ambaye aliahidi kupambana na ufisadi alipochaguliwa kwa mara ya kwanza 2013, haraka alichukua hatua za kupunguza hasira za umma. “Hatutawavumilia watu wasiowaaminifu. Watu waliokabidhiwa majukumu lazima wawe tayari kutumikia badala ya kutumikiwa,” alisema Jumatatu

    Wakosoaji wake wanasema, Kenyatta ambaye alishinda kiutata muhula wa pili mwaka jana amekuwa mlegevu kuwafuatilia viongozi wa juu. Hakuna viongozi wowote wa ngazi ya juu ambao wamechukuliwa hatua tangu alipoingia madarakani.

    Kashfa ya ufisadi imezingira katika Shirika la Taifa la Huduma ya Vijana (NYS), taasisi ya kijeshi ambayo inawafundisha vijana na kuwapeleka kwenye miradi inayoanzia ujenzi hadi udhibiti wa usalama barabarani. Mradi huo umekuwa kipaumbele katika mpango wa Kenyatta kukubali ukosefu wa ajira wa vijana.

    Mkurugenzi mkuu wa mashtaka amesema anafanyia uchunguzi ankara mbalimbali za malipo yanayofikia shilingi za Kenya 8 bilioni (pauni 59 milioni). Uchunguzi wa awali unaonyesha malipo ya ankara nyingi yamezidishwa.

    Vyombo vya habari vya Kenya vimeonyesha kwamba NYS lilitumia dola 10 milioni kulipia nyama kwa mwaka mmoja ikiwa na maana kwamba kila kuruta alikuwa anakula kilo 66 za nyama kwa siku.

    Ankara nyingine, vyombo vya habari vimeandika tairi moja ilinunuliwa kwa dola 1 milioni.

    Chanzo: Mwananchi

    Updates>>>>>>>>

    Washukiwa 20 kati ya 50 waliokuwa wamekamatwa kutokana na sakata ya ufujaji wa Sh8 bilioni ($78m) kutoka kwa Shirika la Vijana wa Huduma kwa taifa (NYS) nchini Kenya wamefikishwa kortini.

    Miongoni mwa walioshtakiwa ni Katibu Mkuu wa wizara ya masuala ya vijana na jinsia Lilian Mbugua Omollo na mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bw Richard ndubai.

    Aidha, mameneja wa kampuni ambazo zinadaiwa kuhusika katika ufujaji wa pesa hizo walifikishwa kortini Milimani, Nairobi.

    Wanatarajiwa kujibu mashtaka mbalimbali yanayohusiana na kutoweka kwa $milioni 5 kati ya takriban dola milioni 80 zilizopotea katika shirika hilo la NYS.

    Kenya.png

    Miongoni mwa mashtaka ambayo wamefunguliwa, ni makosa ya ulaghai, kutumia vibaya mamlaka na kula njama ya kutekeleza ufisadi.

    Washukiwa zaidi wanatarajiwa kufikishwa kortini.

    Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP) Bw Noordin Haji, alikuwa Jumatatu ametangaza kwamba idara yake itawafungulia mashtaka watumishi 40 wa umma na wafanyabiashara 14, pamoja na kampuni 10.

    Awali Haji alisema kuwa upande wake utaiomba mahakama isiwaachie kwa dhamana kwa wakati huu kuzuiwa jitihada zozote za uchunguzi wa kesi hiyo kuingilia kwa namna yoyote.

    Wakenya wanaizungumziaje kesi
    #MoneyLaunderingBanks na #NameTheRealNYSThieves ni mada mbili kuu zinazozungumziwa pakubwa katika mitandao ya kijamii Kenya hususan katika Twitter zikigubika mazungumzo kuhusu mabenki yaliotumika nchini kufanikisha malipo kwa makampuni kadhaa yaliohusishwa katika kashfa hiyo ya takriban dola milioni 80.

    Jamaa huyu katika ujumbe wake hapa anasema hii sio sura mtu anayoweka wakati anajua ataadhibiwa kwa uhalifu.



    Wengine kama huyu wakizungumzia uwakilishi wa washukiwa hao kutokana na anachokitaja kuwa idadi kubwa ya mawakili wa washukiwa dhidi ya anayewasilisha kesi dhidi yao



    Utakatishaji wa fedha
    Gavana wa Benki Kuu ya Kenya amesema huenda baadhi ya benki zilikiuka sheria za kukabiliana na utakatishaji wa fedha katika kutolewa kwa fedha ambazo zinadaiwa kuibiwa kutoka kwa NYS.

    Bw Patrick Njoroge amesema benki hiyo inashirikiana na polisi katika uchunguzi wa wizi huo wa karibu $100m.

    Shirika la NYS limekuwa likishirikishwa sana katika mpongo wa serikali ya Kenya wa kukabiliana na ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana.

    Chanzo: BBC Swahili

    No comments:

    Loading...

    AJIRA

    SIMU

    AFYA

    UDAKU