HABARI BURUDANI MICHEZO UDAKU AJIRA MUZIKI NA MENGINE MENGI KWENYE UKURASA HUU

  • Breaking News

    Wednesday, May 30, 2018

    Serikali ya TZ yashinda kesi dhidi ya wanablogi



    Serikali ya Tanzania, Jumanne ilishinda kesi dhidi ya wanablogi na wanaharakati waliokuwa wanapinga utekelezaji wa kanuni mpya za zinazowataka wamiliki wa mitandao kujiandikisha kwa serikali na kutangaza wafadhili wao.
    Mapema mwezi huu, asasi sita za kiraia ziliwasiilisha hoja mahakamani nay a kutaka kuanza kutekelezwa kwa kanuni hizo kusitishwe kwa muda. Wanaharakati wameushutumu uamuzi huo wa jana na kuutaja kama shmbulizi dhidi ya uhuru wa kujieleza.
    Kanuni hizo mpya zinawataka wamiliki wa mitandao kulipa ada ya hadi dola $90 za Kimarakani, kutoa habari za wajasiriamali, uraia wa wamiliki, tajiriba ya wafanyakazi kati ya mendgine.
    Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, watakaokiuka kanuni hizo huenda wakafungwa jela kwa miezi 12, kupigwa faini ya shilingi milioni tano au adhabu zote mbili.
    Tayari wamiliki wa mitanfdo na tovuti mbalimbali wameanza kuzifunga kwa kuhofia kukamatwa.
    Baadhi ya wanaharakati wanamshutumu rais wa nchi hiyo, John Pombe Magufuli, na kusema kuwa utawala wake unacghukua hatua hiyo kwa sababu unaogopa kukosolewa.
    Magufuli aliingia mamlakani mwaka wa 2015 kwa ahadi kwamba angeharakisha juhudi za kuimarisha uchumi na kukabilina na ufisadi nchini humo.

    No comments:

    Loading...

    AJIRA

    SIMU

    AFYA

    UDAKU