HABARI BURUDANI MICHEZO UDAKU AJIRA MUZIKI NA MENGINE MENGI KWENYE UKURASA HUU

  • Breaking News

    Wednesday, May 30, 2018

    Mugabe akabiliwa na kifungo jela - Bunge



    Bunge la Zimbabwe lilisema Jumatatu kwamba aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Robert Mugabe, anakabiliwa na kifungo gerezani iwapo hatajiwasilisha mbele ya kamati ya bunge inayochunguza shutuma za ufujaji wa dola bilioni 15 za ushuru uliotoka kwa mauzo ya Almasi.
    Baada ya kumsubiri rais huyo wa zamani kwa Zaidi ya nusu saa, ina kukosa kufika mbele ya kamati hiyo ya madini na kawi bila, mwenyekiti wake, Temba Mliswa, alisema kuwa uvumilivu wa wabunge ulikuwa umefika mwisho.
    Msilwa alisema: "Katika barua tunayomwandikia, ambayo ni ya mwisho, tunamkumbusha kwamba tutakuwa tunamwita kufika mbele ya kamati hii, na tunatumai kwamba haitatubidi kuchukua hatua ya kumlazimisha rais wa zamani kufika mbele yetu.
    "Tunatumai kwamba barua hii ya mwisho itakuwa kitu ambacho atafurahia. Iwapo hatafika mbele ya kamati hii, atakuwa amedharau bunge…na kuna athari kadhaa za kufanya hivyo. WachaHebu wakumbusheni kwamba mbunge Roy Bennet, ambaye kwa sasa ni marehemu, alifungwa jela kwa ushauri wa bunge. Kwa hivyo tusisahau nguvu za bunge hili," aliongeza mwenyekiti huyo.
    Hii ni mara ya pili kwa Mugabe, mwenye umri wa miaka 94, kukosa kufika mbele ya kamati hiyo ili kujibu maswali.​
    Kamati hiyo inachunguza shutuma za ufisadi katika seka ya madini aina ya almasi. Mnamo mwaka wa 2016, Mugabe na Zimbabwe walipoteza dola bilioni 15 kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ufujaji katika sekata hiyo.
    Madini ya almasi yaligunduliwa nchini Zimbabwe mnamo mwaka wa 2006 na kuleta matumaini kwamba uvumbuzi huo ungesaidia kuimarisha pakubwa uchumi wan nchi hiyo uliodorora mno.
    Lakini ni ushuru mdogo sana uliowafikia wananchi wa kawaida au hata serikali.
    Ingawaje utawala wa Mugabe uliyashutumu makampuni ya kuchimba madini kwamba hayakueleza faida yaliyokuwa yakipata, shirika la Global Witness na mashirika mengine ya uangalizi wa ufisadi yalieleza wasiwasi juu ya matumizi mabaya ya fedha katika sekta hiyo ya madini.
    Global Witness ilizilaumu idara za usalama na washirika wa kisiasa wa Mugabe kuwa walipora na kuhamisha pesa kutoka kwa sekta ya uchimbaji almasi na kuuza mawe hayo yenye dhamani kubwa na kujifaidi na mapato yote yaliyotokana na mauzo ya bidhaa hiyo.
    Mugabe alijiuzulu mwezi Novemba mwaka jana baada ya shinikizo lililoongozwa na jeshi la nchi hiyo, na hajaonekana hadharani tangu wakati huo.
    Mara ya mwisho alipoonekana kwenye runinga, alikuwa akiwahutubia wanahabari mapema mwaka huu na kumshutumu aliyekuwa makamu wake, ambaye sasa ni rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnagagwa, kwamba alimwondoa mamlakani kwa njia ya mapinduzi.

    No comments:

    Loading...

    AJIRA

    SIMU

    AFYA

    UDAKU