HABARI BURUDANI MICHEZO UDAKU AJIRA MUZIKI NA MENGINE MENGI KWENYE UKURASA HUU

  • Breaking News

    Tuesday, May 29, 2018

    Mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich amepewa uraia nchini Israel.



    Mmiliki wa klabu ya Chelsea Roman Abramovich amepewa uraia nchini Israel.
    Imedaiwa kuwa Abramovich amefikia maamuzi ya kuhamia Israel baada ya Uingereza kumcheleweshea Visa katika kinachoonekana kuchangia zaidi ni mzozo wa kidplomasia uliopo kati ya Uingereza na Urusi.
    Bilionea wa Urusi ambaye ni mmiliki wa klabu ya soka ya Chelsea ya England Roman Abramovich, mwenye umri wa miaka 51, amesafiri kwa ndege hadi Tel Aviv baada ya kupata uraia wa Israel na atakua ndiye mtu tajiri zaidi nchini Israel kwa sasa.
    Bw. Abramovich atakua ni mtu tajiri zaidi nchini Israeli
    Bilionea wa Urusi ambaye ni mmiliki wa klabu ya soka ya Chelsea ya England Roman Abramovich, amesafiri kwa ndege hadi Tel Aviv baada ya kupata haki ya uraia wa Israel. Alikabiliwa na tatizo la kupata upya viza nchini Uingereza katika kinachoonekana kuwa na uhusiano na mzozo wa kidiplomasia kati ya Uingereza na Urusi.
    Mzozo huo ulichangiwa zaidi na kupewa sumu kwa jasusi wa zamani na binti wake Sergei na Yulia Skripal.
    Msemaji wa Abramovich hakutaka kuzungumza lolote kuhusiana na uraia wake mpya aliopewa katika taifa hilo la Mashariki ya Kati.
    Bw Abramovich, mwenye umri wa miaka 51, atakua ndiye mtu tajiri zaidi nchini Israel sasa.
    Viza yake ya uwekezaji nchini Uingereza inaripotiwa kuisha muda wake wiki kadhaa zilizopita, lakini serikali ya Uingereza imekataa kutoa kauli yoyote kuhusiana na 'suala lake binafsi'.
    Kucheleweshwa kwa utoaji wa viza mpya ya Bw Abramovich kunakuja wakati kukiwa na uhasama wa kiplomasia baina ya serikali za London na Moscow Baada ya kupewa sumu kwa jasusi wa zamani wa Urusi Sergei Skripal kusini mwa Uingereza.

    No comments:

    Loading...

    AJIRA

    SIMU

    AFYA

    UDAKU