HABARI BURUDANI MICHEZO UDAKU AJIRA MUZIKI NA MENGINE MENGI KWENYE UKURASA HUU

  • Breaking News

    Wednesday, May 9, 2018

    JE!! Rais Magufuli yuko sahihi katika hili la mikopo chuo kikuu

    JE!! Rais Magufuli yuko sahihi katika hili la mikopo chuo kikuu

    MAGUFULI HAWEZI KUWA SAHIHI KATIKA HILI LA MIKOPO.

    Kabla ya kuanza kujadili kauli hii ya Rais kwanza niorodheshe #interesting_facts katika swala hili.

    1. Je uliwahi kujua kamba pesa inayotumika kusomesha wanafunzi vyuo vikuu na VETA ni pesa inayotolewa na shule binafsi ikiwemo na makampuni mengine binafsi?

    Kodi ya kusomeshea watanzania inaitwa Skills and Development Levy(SDL).

    Kodi zingine zote unazozijua na usizozijua hazihusiki kusomeshea wanafunzi chuo kikuu na VETA.

    Hii kodi hailipwi na kila mtanzania kama kodi zingine bali inalipwa na private schools pamoja na makampuni mengine binafsi.

    Kwa hiyo shule zote binafsi nchini zikishirikiana na makampuni binafsi ndizo zimepewa jukumu la kusomesha wanafunzi chuo kikuu na VETA.

    did you know this?

    Kwa hiyo wanafunzi wote wanaosoma shule binafsi kimsingi ndio wanalipa pesa ya kusomeshea wanafunzi wa chuo kikuu na VETA.

    Pia wanafunzi wote waliowahi kusoma shule binafsi nao walichangia kusomesha wanafunzi vyuo vikuu.

    2. Si kila anayesoma private school kwao ni matajiri.

    Ni muhimu tukajua sababu za msingi wazazi kupeleka watoto shule binafsi ili tuboreshe shule zetu za serikali kuondoa aibu hii.

    wengi wanawapeleka watoto private kwa sababu wana uhakika watoto watapata elimu bora na watafaulu lakini pengine wanasoma kwa shida sana.

    Kumpeleka mtoto serikali moja kwa moja anakosa elimu bora na hata kufaulu linabiki swala la kumwachia mwenyezi Mungu.

    Kwa hiyo kusomesha private si kwa sababu ya jeuri ya pesa.

    (a):Wapo wanaouza mashamba kusomesha.

    (b)wapo wanaouza machungwa na ngogwe kusomesha.

    (c)wapo wanaofanya vibarua kusomesha.

    (d) wapo wanaofanya umachinga kusomesha.

    (e) wapo wanaouza kila kitu nyumbani ikiwemo nyumba ya kuishi ili mtoto aende shule.

    Kuna familia zingine mpaka mtoto anamaliza form four wanakuwa wameuza kila kitu nyumbani.

    (f) wapo wanaosomeshwa na mashirika, ndugu ama marafiki katika shule hizi za private.

    (g) lakini pia kuna private schools zenye gharama nafuu, kiasi kwamba mzazi yeyote aliyedhamiria anaweza kusomesha private kwa kulipa ada kidogokidogo na tena mtoto akawa day.

    (h) kuna watoto wengine ambao ni kweli wametoka familia zenye uwezo ndio maana wakasoma private schools.

    lakini uchumi wa wazazi ukayumba ama wakafilisika, ama biashara ikayumba, ama mzazi amestaafu ama amefukuzwa kazi nk nk.

    Huyu mtoto ambaye amekuwa masikini leo unamnyimaje haki ya kupata mkopo kisa jana alikuwa tajiri?

    Ama ndio kutaka matajiri waishi kama mashetani?

    Kwa hiyo kusoma private si ushahidi kwamba mtu anapesa nyingi kuweza kujisomesha chuo kikuu.

    3. Pia, Si kweli kwamba ukisoma shule za serikali basi wewe ni masikini. Hiki ni kiwango kidogo kabisa cha kufikiri.

    Wapo wazazi ambao wana pesa kabisa lakini wanaamua tu kupeleka watoto shule za serikali.

    Tena wengine waliposikia ukisoma private hupati mkopo basi huamua kuwapeleke watoto serikalini lakini kwa tahadhari kubwa ya kuhakikisha wameajiri mwalimu wa kumfundisha mtoto ili asipate yale masifuri.

    Wengine wanahakikisha wanawalipia watoto tuition za mtaani pesa nyingi wasipate masifuri.

    Wanafanya hivi ili mwisho wasije kukosa mkopo chuo kikuu.

    Tunahitaji kufikiri zaidi.

    4. Wazazi wengi wanapeleka watoto wao private kwa sababu wanaogopa ubovu wa shule za serikali.

    Mbunge wa Ulanga Goodlack Mlinga aliwahi kumwita waziri elimu Profesa Ndalichako kuwa ni waziri wa masifuri(maana shule za serikali zilizo chini yake ndio zinatoa division zero za kutosha)

    Ndio maana akampachika jina la waziri wa masifuri.

    kama tukiondoa matokeo yote ya shule za private basi Ndalichako anageuka kutoka kuwa waziri wa elimu mpaka kuwa waziri wa masifuri.

    Haya masifuri ya shule za serikali kila mtu anayaogopa kuanzia mzazi mpaka mwanafunzi.
    .
    .
    Kwa hiyo tusiwahukumu wanaosoma shule za private na badala yake tujikite kuboresha elimu ya shule zetu za serikali ili tuondokane na aibu hii.
    .
    .
    sasa nirudi kwenye hoja kujadili hatari ya hii kauli.

    Serikali ya Magufuli inaenda kupanda mbegu mbaya ya ubaguzi na uvunjaji haki za mwanafunzi kupata elimu.

    Haiwezekani kwamba pesa yote ya kusomeshea wanafunzi vyuo vikuu itolewe na shule binafsi na makampuni yasiyo ya serikali lakini serikali hiyo hiyo ikatae kuwasomesha wale waliochangia kupatikana kwa hiyo pesa tena wengine ni masikini kweli kweli waliosomeshwa kwa kuuza mashamba yote nyumbani, nyumba ama hizi biashara ndogondogo kama mama ntilie nk.

    Hii ni taarifa ya kushitusha sana.

    Huu ni ubaguzi mkubwa ambao haupaswi kabisa kufumbiwa macho.

    Mathalani Katika ripoti ya CAG ya 2016/2017 iliyoandikwa kwa lugha ya kiingereza,

    katika ukurasa wa 373 imeonesha kwamba kodi ya SDL iliyokusanywa kwa mwaka 2016/2017 ilikuwa zaidi ya billioni 280.

    Katika pesa zote hizo, billioni 93 ndizo zilitumika kugharamia mafunzo yote ya VETA nchini katika vyuo vyote vya serikali.

    Billioni 186 ndizo zilitumika kusomesha wanafunzi chuo kikuu nchini katika mwaka wa masomo 2016/2017. Soma mwenyewe ujionee katika ripoti ya CAG.

    Kwa nini iwe dhambi leo kusoma shule binafsi?

    Kwanza ilibidi tuzishukuru sana shule binafsi kwa kutusomeshea watoto wa taifa hili kwa kugharamia elimu yote ya VETA na mikopo ya chuo kikuu.

    Nini mchango wa shule binafsi nchini?

    Ni ukweli ulio wazi kabisa kwamba shule za private ndizo zinachangia upatikanaji wa wataalamu wa sayansi kwa zaidi ya asilimia 90 nchini.

    Hivi leo karibu wanafunzi wote wanasoma sayansi waliopo shule za serikali A level ni zao la shule binafsi.

    Kama si O level basi A level. Sitaki kuingia ndani sana katika hili.

    Kwa lugha rahisi ni kwamba bila shule za private hivi leo tungekosa madaktari na tungekosa wahandisi.

    Na vyuo vyetu vya sayansi na uhandisi vingekumbwa na uhaba mkubwa mno wa wanafunzi.

    Wanafunzi wasibaguliwe katika mikopo.

    Ni mara nyingi sana nimekuwa napinga hata utaratibu wa kupendelea tu wanafunzi wa sayansi huku wale wa kozi za arts wakitelekezwa kana kwamba taifa haliwahitaji.

    Wanafunzi wote wapewe mikopo iwe ni wale waliosoma private schools ama masomo ya arts kama waliosoma shule za serikali na masomo ya sayansi.

    Nawasilisha 


    chanzo:jamiiforus

      https://www.jamiiforums.com/threads/rais-magufuli-hawezi-kuwa-sahihi-katika-hili-la-mikopo-chuo-kikuu.1440677/

    No comments:

    Loading...

    AJIRA

    SIMU

    AFYA

    UDAKU