HABARI BURUDANI MICHEZO UDAKU AJIRA MUZIKI NA MENGINE MENGI KWENYE UKURASA HUU

  • Breaking News

    Friday, May 18, 2018

    Kama ulikua humjui vizuri Rais John Magufuli ngoja nikufahamishe;-


    - Jina lake halisi anaitwa John Pombe Joseph Magufuli,
    - Amezaliwa tarehe 29/10/1959,
    - Sehemu alizaliwa ni Chato Geita,
    - Mke wake anaitwa Janeth,
    - Anawatoto 3,
    - Dini mkristo na dhehebu lake ni Mkatoliki,
    - Kabila lake Msukuma,
    - Mwaka 1967 alianza shule ya msingi iitwayo Chato primary iliopo mkoani Geita na kumaliza Mwaka 1974,
    - Mwaka 1975 - 1978 alisoma shule ya sekondari iitwayo Lake Nyanza iliopo Mwanza,
    - Mwaka 1979 hadi 1981 alisoma Mkwawa high school iliopo Iringa,
    - Mwaka 1981 hadi 1982 alienda kusoma diploma ya ualimu katka chuo cha ualimu kiitwacho Mkwawa Education College na alikua anasoma Masomo mawili tu yaani Kemia na Hisabati,
    - Mwaka 1982 alipo makiza tu kusoma aliajiliwa na kufundisha shule ya msingi Sengerema iliopo mkoani Mwanza na alikua anafundisha kemia na Hisabati Mpaka mwaka 1983,
    - Mwaka 1983 - 1985 alienda kupata mafunzo ya JKT huko Dodoma katika Kambi ya Makutopola,
    - Mwaka 1985 hadi 1988 alisomea degree ya kwanza ya elimu katka chuo kikuu cha dar es salaam na alikua anasoma masomo mawili tu yaani Kemia na Hisabati na kutunukiwa shahada ya kwanza,
    - Mwaka 1989 hadi 1990 alikua mkemia mkuu wa chama cha ushirika cha Nyanza,
    - Mwaka 1991 hadi 1994 alisomea shahada ya pili yaani (Masters) ya kemia katika chuo kikuu dar es salaam na baadae akapata ufadhili na kwenda kumalizia Uingereza na kutunukiwa shahada ya pili yaani Masters ya kemia,
    - Mwaka 1995 alijiingiza kwenye siasa na kugombea Ubunge katka jimbo Chato na kushinda,
    - Alikua mbunge wa kawaida kwa miaka mitano yaani 1995 hadi 2000 ambapo baada ya hapo aliteuliwa na Mkapa kuingia kwenye baraza lake la mawaziri,
    - Mwaka 2000 hadi 2005 aliteuliwa na mkapa kuwa Naibu Waziri wa Ardhi na maendeleo ya Makazi,
    - Mwaka 2005 hadi 2008 aliteuliwa na kikwete kuwa waziri wa ardhi na maendeleo ya makazi,
    - Akiwa waziri wa ardhi mwaka 2006 alisoma shahada ya tatu ya kemia kwa njia ya masafa yaani distance learning na kumaliza Mwaka 2009 na kutunikiwa shahada ya tatu yaani Phd ya kemia,
    -Mwaka 2008 hadi 2010 aliteuliwa kuwa waziri wa Mifugo na Uvuvi,
    -Mwaka 2010 hadi 2015 aliteuliwakuwa waziri wa ujenzi,
    -Mwaka 2015 alichukua fomu ya kugombea Urais na kufanikiwa kushinda kwa aslimia 58.46%.
    Huyo ndio John Magufuli rais wa Tanzania kwa sasa.
    Neno moja kwake....

    No comments:

    Loading...

    AJIRA

    SIMU

    AFYA

    UDAKU