Msanii wa muziki Bongo kutokea kwenye label ya WCB, Harmonize amefunguka kuwa kolabo yake na Diamond inayokwenda kwa jina la Kwa Ngwaru mwanzo alipanga kufanya na Davido kutoka Nigeria.
Muimbaji huyo katika mahojiano na kipindi cha Uhondo, E FM amesema wakati aki-shoot video yake ya ngoma ‘Shulala’ nchini Nigeria alikutana na Dj mmoja akamwambia wafanye ngoma na Davido ambayo ataisimamia yeye.

Hata hivyo amesema kwa kipindi hicho Davido alikuwa ameenda nchini Marekani lakini Dj huyo alimueleza kuwa anaweza kuanza kurekodi ndipo alipoanza na alipoondoka Nigeria alikuja na ngoma hiyo Bongo hadi Wasafi Records kwa producer Laizer.
“Wakati narekodi Diamond alikuwa ofisini akaipenda akaanza kuandika verse yake huko huko akaja akaniambia project kali sana. Nikamwambia nataka kufanya na Davido,” amesema Harmonize.
Amesema mara baada ya Diamond kusikia kauli hiyo akamwambia akifanya na Davido itamsaidi sana Afrika lakini baadaye Diamond alikuja kuupenda zaidi wimbo huo ndipo walipoamua kufanya pamoja.
Kwa Ngwaru ni kolabo ya pili kwa Harmonize kufanya na Diamond baada ya Bado iliyotoka mwaka 2016.
No comments:
Post a Comment