Promota wa Anthony Joshua, Eddie Hearn anatarajia kukutana na timu ya bondia, Deontay Wilder wiki ijayo kwaajili ya mazungumzo ya pambano lao la ubingwa wa dunia wa uzito wajuu.
Joshua bado anasubiria ofa kutoka kwa WBC king Wilder ambaye bado hajakubaliana na kiasi cha fedha cha Dola za Kimarekani milioni 12.5 ili kuwa tayari kwa mpiganaji huyo wa Uingereza anaemiliki ubingwa wa IBF, WBA na WBO.
Hearn amekiambia chombo cha habari cha Sky Sports kuwa anatarajia kutua nchini Marekani kwaajili ya mazungumzo na watu wa Wilders kwaajili ya kufanikisha pambano hilo.
“Ninakwenda kukutana nao New York, uso kwa uso mimi nao wao na kuangalia kama tunaweza kufanya dili likakamilika,” amesema Hearn.
Hearn ameongeza “Tuliweka ofa wiki iliyopita na hatujajibiwa kitu chochote kutoka kwao. Wiki ijayo tutakuwa huko New York kwasababu kutakuwa pia na pambano kati ya Danny Jacobs dhidi Katie Taylor.”
Bingwa wa WBA, Joshua atautetea mkanda wake huo dhidi ya Alexander Povetkin kabla ya kupambana na Wilder.
No comments:
Post a Comment