Wakati Yanga wakielekea kwenye hatua za mwisho kunasa saini ya kocha, Zahera Mwinyi ‘Mkongoman’ atakaerithi mikoba ya George Lwandamina mabingwa hao watetezi wa ligi kuu soka Tanzania Bara sasa wanaelekeza nguvu zao kwa straika wa Nigeria, Quadri Kola Aladeokun.
Yanga SC ipo kwenye hatua za mwisho kunasa saini ya straika huyo wa Nigeria, Quadri Kola Aladeokun ambaye ni chaguo la kiungo wa timu hiyo Pappy Kabamba Tshishimbi atakaechukua nafasi ya Donald Ngoma.
Taarifa za chini ya kapeti zinasema kuwa awali straika huyo alipaswa kutua nchini jana lakini ikashindikana na hivyo kutarajiwa kutua mapema wiki hii ili kumalizana naye.
Juma lililopita Ngoma amesema kuwa kuna ugumu mtu kutambua kipindi kigumua anachopitia kwenye mchezo wa soka.
Wakati mwingine ni vigumu kujua vipi mtu mwingine anaamini kwenye hali uliyonayo,kwenye soka upo wakati ngumu mchezaji unaweza kuupitia.
Yanga ambayo ipo kwenye mashindano ya kimataifa inatarajia kusajili straika wa kigeni ili kuziba nafasi ya Ngoma ambaye siku zake za kuwemo kwenye klabu hiyo zinahisabika.
No comments:
Post a Comment