HABARI BURUDANI MICHEZO UDAKU AJIRA MUZIKI NA MENGINE MENGI KWENYE UKURASA HUU

  • Breaking News

    Friday, May 18, 2018

    WHO yaweka ilani ya Ebola katika kiwango cha juu DRC



    Shirika la Afya Duniani (WHO) limesema katika tamko lake Ijumaa kuwa limeongeza ilani ya hatari ya ugonjwa wa Ebola kwa afya ya umma uliotokea Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika kiwango cha juu zaidi katika ngazi ya taifa.
    Hatua hiyo imekuja baada ya kesi mpya ya ugonjwa wa Ebola kuthibitishwa katika moja ya kanda tatu za kiafya katika eneo la Mbandaka, mji ambao unazaidi ya watu milioni moja katika jimbo la Kaskazini magharibi la Equateur, ambako ugonjwa huu uligundulika baada ya mlipuko huo mapema mwezi huu.
    WHO imesema itapeleka wataalam 30 kufanya uchunguzi katika mji huo. Shehena ya kwanza ya dawa za kinga za majaribio 4,000 ziliwasili Jumatano katika mji mkuu, Kinshasa.
    WHO pia imeongeza tahadhari hiyo kimkoa kwa kiwango cha “juu” kutoka cha “kati” na kuacha tathmini ya hatari hiyo duniani kuwa ya kiwango cha “chini”.
    Hadi hivi sasa, jumla ya kesi 44 ambazo inawezekana au kushukiwa kuwa ni Ebola zimeripotiwa, vikiwemo sio chini ya vifo 23.
    Mlipuko wa ugonjwa wa Ebola uliotokea mwaka 2014, ambapo zaidi ya watu 11,000 walikufa katika nchi za Afrika Magharibi za Guinea, Liberia na Sierra Leone.

    No comments:

    Loading...

    AJIRA

    SIMU

    AFYA

    UDAKU